Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BARAZA LA MADIWANI USHETU LAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027




Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu leo, Novemba 05, 2026, imefanya Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa siku ya kwanza kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza (Julai–Septemba), katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Katika mkutano huo, Baraza limepokea taarifa za maendeleo kutoka katika kata zote Ishirini (20) za Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, zikielezea hatua za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo, hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na changamoto zilizojitokeza katika kipindi husika.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Mhe. Gagi Lala Gagi, ambapo wajumbe wa Baraza wamepata fursa ya kupitia na kujadili taarifa zilizowasilishwa, kutoa maoni na kuelekeza hatua mbalimbali zinazopaswa kuchukuliwa ili kuimarisha usimamizi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Mkutano huo ni sehemu ya utaratibu wa kisheria na kiutawala unaolenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi na usimamizi wa shughuli za maendeleo, kuhakikisha mipango iliyowekwa inatekelezwa kwa kuzingatia malengo yaliyokusudiwa na kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Ushetu.

Post a Comment

0 Comments