Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZIARA YA NAIBU MEYA KAHAMA NA DIWANI MWENDAKULIMA KUKAGUA MIRADI YA HUDUMA ZA JAMII

Na Neema Nkumbi, Kahama

Naibu Meya wa Manispaa ya Kahama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwendakulima, Mhe. Shaban Mikongoti, leo Mei 19, 2026 wamefanya ziara maalumu pamoja na Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) kutembelea na kukagua huduma katika Kituo cha Afya Mwendakulima, Zahanati ya Mwime pamoja na Shule ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu Mwime.


Ziara hiyo imelenga kufuatilia maendeleo ya huduma za afya na elimu katika kata hiyo, kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha huduma kwa jamii katika maeneo hayo.

Post a Comment

0 Comments