Rais Samia Ampongeza Prof. Mohamed Yakub Janabi kwa Kuchaguliwa Mkurugenzi wa Kanda wa WHO – Afrika
"Natoa pongezi za dhati kwa Profesa Mohamed Yakub Janabi kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Afrika kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.
Kwa uzoefu na ujuzi uliouthibitisha kwa miongo kadhaa katika sekta ya afya, nina imani kubwa kuwa una kila sifa na uwezo wa kulitumikia bara letu na kuliongoza kuelekea mafanikio makubwa zaidi.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashukuru kwa kila nchi mwanachama iliyoiamini taaluma, uzoefu na maono yako kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.
Profesa, nakutakia mafanikio mema katika kipindi chako cha uongozi."

0 Comments