Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PPRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI YA MFUMO WA NeST KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA


NA NEEMA NKUMBI -MSALALA

Meneja PPRA Kanda ya Kati na Magharibi, Mhandisi Suma Atupele, ameongoza mafunzo ya matumizi ya mfumo wa manunuzi wa NeST kwa Watendaji wa kata, vijiji, walimu wakuu, na wagavi, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kuanzia tarehe 17 Machi 2025 hadi 18 Machi 2025.


Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Mhandisi Atupele amewataka watumishi kuhakikisha wanatumia mfumo wa NeST kwa usahihi ili uwe na tija kwa maeneo yao pia amesisitiza kuwa matumizi sahihi ya mfumo huo yatasaidia kupunguza changamoto zinazohusiana na manunuzi katika miradi inayoendelea kutekelezwa.


Watendaji wameeleza kuridhishwa na mafunzo hayo, wakisema kuwa hapo awali walikuwa wakitumia mfumo huo bila uelewa wa kutosha, lakini sasa wamepatiwa mafunzo yaliyowajengea uwezo mzuri na kuahidi kufanya matumizi bora ya mfumo ili kuepuka changamoto zilizokuwepo awali.


Naye Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Ndg. Stanley Manyonyi, amewashauri watumishi hao kutumia mfumo huo kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA, kama inavyoelekeza katika miongozo ya PPRA.

Post a Comment

0 Comments