Manispaa ipo kwenye mchakato wa ukamilishaji wa utengenezaji wa ramani kwa ajili ya kusajiriwa Wizarani na baada ya hapo kupata namba za viwanja hivyo 246 vya wananchi wa mtaa wa Ndala”,ameongeza.
Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga amesema TAKUKURU inaendelea kufuatilia ugawaji wa namba za viwanja vilivyopimwa katika mtaa wa Mlepa mpaka litakapokamilika lakini pia kufuatilia zoezi la ukamilishaji wa uandaaji wa namba za viwanja za mtaa wa Ndala na ugawaji wake.
Hali kadhalika TAKUKURU inaendelea kufanya vikao vya utambuzi wa kero katika kata 14 kutoka kata za Mwenge, Mwawaza, Kolandoto, Lyabukande, Puni, Nyida, Mhongoloi, Majengo, Nyasubi, Ulowa, Bulungwa, Mpunze, Bupigi na Bubiki.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari
0 Comments